Wanaume Mkae Chonjo, Wanawake Wamebumbuluka
Labda mwaweza kufikiri nimeivamia kazi ya Da’Mija kuhusu wanawake na maendeleo yao. Yawezekana ndivyo lakini mtazamo wangu umenituma nifanye hivyo. Ndesanjo naye jana kachokonoa.Kadri dunia ibadilikavyo ndivyo hata mitazamo ya binadamu inabadilika. Hebu fikiri miaka ile ya zamani na sasa hasa katika ulingo wa siasa. Ilikua haba kukuta mwanamke eti yuko ngazi za juu kama vileza uraisi, umakamu wa raisi au hata uwaziri nyeti katika serikali, achilia mbali nchi za kifalme ambapo mtu anawezajikuta yu malkia ama mfalme midhali kazaliwa katika ukoo ama familia ya kifalme. Hata kama hana busara wala akili za kutosha anakua tu, utake usitake. Katika miongo na miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia mabadiliko ya mitazamo ya jinsia katika uwanja wasiasa duniani. Hata Afrika ambako mfumo dume umeshamiri (mfano kule mkoani Mara alikozaliwa Boniface Makene anayeishi Dar es Salaam). Tulikwisha zoea kuhusianisha majukumu ya kiserikali nawanaume. Katu hatukua hata na imani kuwa wanawake nao wanaweza. Sasa dunia imebadilika. Mtu wa jinsia yoyote iwayo anaweza kuwa kiongozi mkubwa tu katika siasa za ulimwengu huu pepe. Mwaka 1994 alianza Bibi Chandrika Kumaratunga wa SriLanka, Mwaka 2001 akafuatia Bibi Gloria Arroyo waPhillipines. Kama vile ndio waliwashamoto msululu wawanawake kutamani kuwa maraisi ukachanua. Hata katikaKenya aliwahi jitokeza Bibi Charity Ngilu lakini ghiliba za siasa za wakati ule katu hazikumwezesha kufua dafu mbele ya profesa Daniel arap Moi.
Wakinamamahawakuishia hapo. Mwaka jana kwa mara yakwanza mwanamama Angela Dorothy Markel, kiongozi yachama cha Christiaan Democratic Union alishinda kiti cha ukansela kule Ujerumani (pichani juu).
Mwaka huo huo mwanamama Ana Claudia Senkoro (pichani kushoto) kwa mara ya kwanza alikua mgombea wa kiti cha uraisi nchini Bongo. Hata hivyo, hakufanikiwa mbele yamidume ile 9 shababi yenye uchu wa Ikulu mithili yanini sijui. Mwaka huo huo 2005 katika mchuano mkali wa uraisi kule nchini Liberia kwa mara ya kwanza mwanamke mchumi Ellen Johnson-Sirleaf (chini ya Senkoro) alimbwaga mwanasoka George Opong Weah na kuwa raisi wa kwanza mwanamke katika Afrika nzima. Kama vile haitoshi kule Afrika ya kusini, baadaya aliyekuwa makamu wa rais Jakob Zuma kufanya maneno mbofumbofu, kwa mara yakwanza katika historia nzito ya nchi hiyo Mwanamama Phumzile Mlambo-Ngcuka aliteuliwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo.
Mwezi huu kwa mara ya kwanza mwanamama Michelle Bachelet (kulia) amefanikiwa kuwa rais wa Chile mwanamke. Hapa Marekani kumekuwa na harakati za aliyekuwa mke wa raisi Clinton, Hillary Rodham Clinton kutamani kugombea na kuwa raisi wa kwanza mwanamke katikahistoria ya Marekani.
Ingawaje kule Bongo Prez Jakaya alishinda lakini nako mabadiliko ya jinsia si haba. Kwa mara ya kwanza katika baraza lake la
mawaziri, ambalo kwa mara ya kwanza ni kubwa kuliko yote katika historia ya Bongo, amewateua wanawake wengi sio tu kuwa mawaziri bali pia kukamata wizara nyeti. Kwa mara ya
kwanzaBibi Zakia Hamdani Meghji (kulia)amekuwa waziri wa kwanza wa pesa mwanamke katika Afrika ya Mashariki. Kwa mara yakwanza mhasibu Ana Makinda (kushoto) ameshinda na kuwa naibu wa Spika wa kwanza mwanamke. Kwa mara ya kwanza Mwanamke mwanasheria Dk Asha-Rose Mtengeti Migiro amekuwa mwanamake wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Kigeni na Ushirikiano waKimataifa.
Mwaka huo huo mwanamama Ana Claudia Senkoro (pichani kushoto) kwa mara ya kwanza alikua mgombea wa kiti cha uraisi nchini Bongo. Hata hivyo, hakufanikiwa mbele yamidume ile 9 shababi yenye uchu wa Ikulu mithili yanini sijui. Mwaka huo huo 2005 katika mchuano mkali wa uraisi kule nchini Liberia kwa mara ya kwanza mwanamke mchumi Ellen Johnson-Sirleaf (chini ya Senkoro) alimbwaga mwanasoka George Opong Weah na kuwa raisi wa kwanza mwanamke katika Afrika nzima. Kama vile haitoshi kule Afrika ya kusini, baadaya aliyekuwa makamu wa rais Jakob Zuma kufanya maneno mbofumbofu, kwa mara yakwanza katika historia nzito ya nchi hiyo Mwanamama Phumzile Mlambo-Ngcuka aliteuliwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo.
Mwezi huu kwa mara ya kwanza mwanamama Michelle Bachelet (kulia) amefanikiwa kuwa rais wa Chile mwanamke. Hapa Marekani kumekuwa na harakati za aliyekuwa mke wa raisi Clinton, Hillary Rodham Clinton kutamani kugombea na kuwa raisi wa kwanza mwanamke katikahistoria ya Marekani.Ingawaje kule Bongo Prez Jakaya alishinda lakini nako mabadiliko ya jinsia si haba. Kwa mara ya kwanza katika baraza lake la
mawaziri, ambalo kwa mara ya kwanza ni kubwa kuliko yote katika historia ya Bongo, amewateua wanawake wengi sio tu kuwa mawaziri bali pia kukamata wizara nyeti. Kwa mara ya
kwanzaBibi Zakia Hamdani Meghji (kulia)amekuwa waziri wa kwanza wa pesa mwanamke katika Afrika ya Mashariki. Kwa mara yakwanza mhasibu Ana Makinda (kushoto) ameshinda na kuwa naibu wa Spika wa kwanza mwanamke. Kwa mara ya kwanza Mwanamke mwanasheria Dk Asha-Rose Mtengeti Migiro amekuwa mwanamake wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Kigeni na Ushirikiano waKimataifa.Kwa mwendo huu dira inaonyesha wanamwake sasa wamebumbuluka baada ya kubumbulushwa. Na sasa hawasikii la mtu. Usawa kwa kwenda mbele. Enyi walume mnaofikiria kuingia katika siasa upinzani sasa ni waaina tatu: mosi dhidi ya wapinzani ndani ya chama, pili dhidi ya wapinzani nje ya chama, tatu dhidiyawanawake ndani na nje ya chama.