Thursday, January 19, 2006

Safari ya Alabama Ilifana Sana
Bila shaka wanablogu wa Kiswahili mmekuwa mkinikosa au kunimiss kwa wakati fulani hivi. Matatizo ya kiufundi yalinifungia nje ya ulimwengu wa blogu. Si shaka baadhi yenu mlikuwa mnafahamu nilikuwa Marekani ya kusini kule Hoover, Alabama kwa rafiki yangu Geofrey Mwaituka, ninayeonekana naye kwenye baadhi ya picha hizi. Huyo mwenje sweta jekundu ni mtoto wa Ilala Tonny Igata.

Hakika safari ya Alabama ilikuwa ‘bomba mbaya’ (nzuri). Tofauti na hapa New Jersey nilikorejea usiku wa jana, kule Alabama kuna wabongo kibao. Utafikiri watanzania huwa wanaambiana kuwa wao ‘waendage’ Alabama. Utafikiri hii haitoshi. Hali ya hewa kule ni bomba mbaya kama utaifananisha na hii ya hapa NJ. Kule kuna baridi ya afya sio hii ya dhoruba hapa karibu na New York.

Ingawaje wabongo wale hawatamani kurejea Bongo, hasa hivi karibuni, lakini kati ya majambo waliyonishauri nililipenda hili la kuwa wao hawawezi kurejea Bongo hivi sasa kwani hawajui namna ya kuanza maisha kule kwa Prez Jakaya na hivyo eti kwa kuwa mimi najua namna ya kuishi Bongo ni vema nimalizapo mizunguko ya hapa kwa Joji Kichaka nirejee Bongo. Wanadai ingawaje maisha yao ya hapa mtoni ni poa kinamna lakini wanayakosa maisha ya ndugu, jamaa na marafiki. Eti maisha ya hapa ni ya kikafiri tu. Basi tu kwa kuwa wamesha yazoea. Wafanyeje?

Nimechomekea kiduchu muhtasari wa mtazamo wa maisha ya hapa Marekani ingawaje sio lengo kuu la chapisho hili. Leo natamani kuwasabahi tu. Naona Boniface Makene na Ndesanjo Macha walishaanza-ga kuwa-ga na wasiwasi kuwa huenda nilishapotelea Mexico. Nimerejea na ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya ya ugali wa kule kusini mwa nchi hii. Kublogu kwa kwenda mbele.

7 Comments:

At 12:02 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Kichwa cha habari cha habari hii, kimenikumbusha ule wimbo wa "Safari yeetu Mbeeya...tulifurahi saaana,...wakazi woote Mbeeya walitushangiliiya...."

Hivi uliimbwa na nani vile?

 
At 9:20 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Karibu karibu vibaya kukaa kimya.

 
At 6:07 AM, Blogger mark msaki said...

aksante bwana baragumu, blogu yako iko very interactive....makene saidia lugha hapo!! ....ninaifurahia sana,,,

 
At 6:08 AM, Blogger mark msaki said...

halafu ingekuwa bomba ungepozi na yule bwana aliyeua what da hell da pm is!!

 
At 2:52 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Da'Mija ule wimbo nami nemesahau ulimbwa-ga na nani. Ninachokumbuka ulitumika kuzindua siku ya wakulima 7-7 kule nyumbani kwetu Mbeya, ambayo baadaye makabaila wa Bongo wakaifanya kuwa siku kuu ya biashara.

Hata hivyo wakaanzisha siku nyingine ya kutukumbuka wakulima mwaka 1993 wakaiita 8-8, nayo ikazinduliwa Mbeya. Mbeya kwa kilimo si haba isipokuwa wachuuzi wanatulangua na kutuacha mafukara.

Mark Msaki yule jamaa alikua kazini usiku huo. Si unajua huku Marekani kazi usiku na mchana. hakuna kulala.

 
At 4:13 AM, Blogger mark msaki said...

naelewa, kakobe naye kampa JK changamoto kuhakikisha mizigo inapigwa mchana na usiku....nimecot hiyo link kwenye makala yangu ya weekend globuni...nadhani ni changamoto nzuri!!! siku nyengine akaja basi upige naye picha tumuone!!

safari yetu mbeya ilipigwa nadhani na Marquise Original wakati huo nadhani aliyeimba ni King Kiki Du Zaire mzee wa kitambaa cheupe siku hizi! wakati huo walikuwa wanacheza chekecha cheke chekeecha cheke! cheza kwa maringo chekecha cheke...

hizi ishu nyingine huyu bwna anaitwa Mtimkubwa ni Enclyopadia...sijui kama nimepatia kuandika...musimuone vile yule Mti mkubwa kweli kweli...na michuzi aliishaongezea Mkavu!!!

cheers

 
At 1:29 PM, Blogger iman rahman said...

I like it this really good information
Vimax Canada

 

Post a Comment

<< Home