Tuesday, January 24, 2006

Wanaume Mkae Chonjo, Wanawake Wamebumbuluka

Labda mwaweza kufikiri nimeivamia kazi ya Da’Mija kuhusu wanawake na maendeleo yao. Yawezekana ndivyo lakini mtazamo wangu umenituma nifanye hivyo. Ndesanjo naye jana kachokonoa.
Kadri dunia ibadilikavyo ndivyo hata mitazamo ya binadamu inabadilika. Hebu fikiri miaka ile ya zamani na sasa hasa katika ulingo wa siasa. Ilikua haba kukuta mwanamke eti yuko ngazi za juu kama vileza uraisi, umakamu wa raisi au hata uwaziri nyeti katika serikali, achilia mbali nchi za kifalme ambapo mtu anawezajikuta yu malkia ama mfalme midhali kazaliwa katika ukoo ama familia ya kifalme. Hata kama hana busara wala akili za kutosha anakua tu, utake usitake. Katika miongo na miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia mabadiliko ya mitazamo ya jinsia katika uwanja wasiasa duniani. Hata Afrika ambako mfumo dume umeshamiri (mfano kule mkoani Mara alikozaliwa Boniface Makene anayeishi Dar es Salaam). Tulikwisha zoea kuhusianisha majukumu ya kiserikali nawanaume. Katu hatukua hata na imani kuwa wanawake nao wanaweza. Sasa dunia imebadilika. Mtu wa jinsia yoyote iwayo anaweza kuwa kiongozi mkubwa tu katika siasa za ulimwengu huu pepe. Mwaka 1994 alianza Bibi Chandrika Kumaratunga wa SriLanka, Mwaka 2001 akafuatia Bibi Gloria Arroyo waPhillipines. Kama vile ndio waliwashamoto msululu wawanawake kutamani kuwa maraisi ukachanua. Hata katikaKenya aliwahi jitokeza Bibi Charity Ngilu lakini ghiliba za siasa za wakati ule katu hazikumwezesha kufua dafu mbele ya profesa Daniel arap Moi.
Wakinamamahawakuishia hapo. Mwaka jana kwa mara yakwanza mwanamama Angela Dorothy Markel, kiongozi yachama cha Christiaan Democratic Union alishinda kiti cha ukansela kule Ujerumani (pichani juu).
Mwaka huo huo mwanamama Ana Claudia Senkoro (pichani kushoto) kwa mara ya kwanza alikua mgombea wa kiti cha uraisi nchini Bongo. Hata hivyo, hakufanikiwa mbele yamidume ile 9 shababi yenye uchu wa Ikulu mithili yanini sijui. Mwaka huo huo 2005 katika mchuano mkali wa uraisi kule nchini Liberia kwa mara ya kwanza mwanamke mchumi Ellen Johnson-Sirleaf (chini ya Senkoro) alimbwaga mwanasoka George Opong Weah na kuwa raisi wa kwanza mwanamke katika Afrika nzima. Kama vile haitoshi kule Afrika ya kusini, baadaya aliyekuwa makamu wa rais Jakob Zuma kufanya maneno mbofumbofu, kwa mara yakwanza katika historia nzito ya nchi hiyo Mwanamama Phumzile Mlambo-Ngcuka aliteuliwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo.

Mwezi huu kwa mara ya kwanza mwanamama Michelle Bachelet (kulia) amefanikiwa kuwa rais wa Chile mwanamke. Hapa Marekani kumekuwa na harakati za aliyekuwa mke wa raisi Clinton, Hillary Rodham Clinton kutamani kugombea na kuwa raisi wa kwanza mwanamke katikahistoria ya Marekani.

Ingawaje kule Bongo Prez Jakaya alishinda lakini nako mabadiliko ya jinsia si haba. Kwa mara ya kwanza katika baraza lake la mawaziri, ambalo kwa mara ya kwanza ni kubwa kuliko yote katika historia ya Bongo, amewateua wanawake wengi sio tu kuwa mawaziri bali pia kukamata wizara nyeti. Kwa mara ya kwanzaBibi Zakia Hamdani Meghji (kulia)amekuwa waziri wa kwanza wa pesa mwanamke katika Afrika ya Mashariki. Kwa mara yakwanza mhasibu Ana Makinda (kushoto) ameshinda na kuwa naibu wa Spika wa kwanza mwanamke. Kwa mara ya kwanza Mwanamke mwanasheria Dk Asha-Rose Mtengeti Migiro amekuwa mwanamake wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Kigeni na Ushirikiano waKimataifa.
Kwa mwendo huu dira inaonyesha wanamwake sasa wamebumbuluka baada ya kubumbulushwa. Na sasa hawasikii la mtu. Usawa kwa kwenda mbele. Enyi walume mnaofikiria kuingia katika siasa upinzani sasa ni waaina tatu: mosi dhidi ya wapinzani ndani ya chama, pili dhidi ya wapinzani nje ya chama, tatu dhidiyawanawake ndani na nje ya chama.

19 Comments:

At 1:06 PM, Blogger Boniphace Makene said...

Hongera baragumu umekuja kwa staili kali sana, Hizo picha zimependezesha sana makala hii na kuipa taswira chanya ya usomaji. Lakini utani sasa, pale kwa Mark Msacky kuna hao hao vipi kuhusu hilo au hujko nako ni kuamka?

 
At 6:11 AM, Blogger mark msaki said...

karibu sana bwana mwaipopo, makene hajaongopa nimehifadhi wahabeshi shoo rumu pale kwangu karibu sana..

 
At 11:13 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Mwaipopo hali hii tunaweza kuifananisha na upandaji wa mti hadi uzao wa mti ule.

Kwamba tunaanza kuwa na mbegu, halafu tunaipanda kisha huchipua kama mmea ambao nao hukua hadi kuzaa matunda. Sasa ndio hali halisi ya kinamama na uongozi wakati huu, wazo la wanawake kuchukua nafasi lilipandwa zamani lilikuwa bado halijazaa matunda kwa vile lilikuwa katika mchakato wa kukua yaani kukabiliana na mtizamo uliopo katika jamii kwamba mwanaume ndio kila kitu, kadiri wakati unavyokwenda jamii nayo inaanza kukubaliana na uwezo wa wanawake katika uongozi hadi kufikia kuwapa nafasi hali hii ndio tunaweza kuiita uzazi wa matunda. Kwa hiyo tunaweza kusema lilikuwa ni suala la wakati tu.
Hata hivyo tunamshukuru Mungu kwa kuilinda mbegu hadi kuzaa matunda maana kuna mengi yapitayo wakati wa ukuaji.

 
At 5:09 AM, Blogger mloyi said...

Kumbuka wakati wa Malkia Nzinga na Malkia wa Sheba.
Tafuta tofauti zao na za hawa wanaojitia kimbelembele sasa. Sijui kama wanatafuta kisasi au ni nia ya kujichanganya tu na kuonyesha kazi uwezo wao. Bush na marekani hasemi kitu ingawa wao ni vinara wa demokrasia, cha kushangaa wanapigania viinchi vidogodogo kuwa na maraisi wanawake wakati wao hawafikirii kitu kama hicho, tena tafuta lengo lao! Kama ni zuri na dunia iwe nzuri ila kama ni baya, nao waendelee kuwa wabaya.

 
At 12:50 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Mloyi umenikumbusha Malkia Nzinga, kweli alikuwa ni moto wa kuotea mbali. Kwa habari yake zaidi ipate hapa.. http://www.damija.blogspot.com/2005/05/malkia-nzinga-mbande-wa-angola.html

 
At 6:22 AM, Blogger Bwaya said...

ee bana ee, hii staili yako ya uandishi ni bomba mbaya yaani! Kazi nzuri sana!
Kuhusu huu "mbumburuko" (sijui kama nikiswahili au nini vile), nadhani akina mama zetu wameamua kutoa mchango wao moja kwa moja katika siasa. Hili ni jambo la kupongeza sana, ingawa kimsingi bado tunahitaji mabadiliko ya kweli.
Walinyanyaswa sana akina mama, waache nao watese bwana! We fikiria, Mungu mwenyewe anaaminika kuwa ni "he" yaani dume!...

 
At 10:31 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Safi ulivyotupangia picha. Lakini tusije wasahau akina Yaa Asantewaa, Mbuya Nehanda, na wengine ambao walijitokeza enzi ambazo hakuna mtu aliyewaza mkutano kama ule wa Beijing. Pia akina Indira Gandhi.

Hili suala la kubadilika kwa mtazamo wa binadamu ni muhimu sana. Kila baada ya miaka mingi katika historia yetu huwa kunatokea mabadiliko makubwa kutokana na mabadiliko ya mtazamo. Yanaweza kuwa mabadiliko mapya au marudio ya mambo ambayo yalishatokea huko nyuma. Unajua historia ina tabia ya kwenda mbele na kurudi nyuma wakati huo huo. Ibn Khaldun, yule baba wa sosholojia toka Afrika ya Kaskazini ameandika sana juu ya mwendo huu wa historia.

 
At 11:49 AM, Blogger Indya Nkya said...

Kwa vile kwa miaka mingi wanaume wamekuwa walitawala na Kwa Afrika hatujaona mabadiliko ni vizuri tuwape kina mama nafasi ili wasaidie nao.

 
At 9:43 AM, Blogger Michuzi said...

hizo bia mloshika ni heinekeni nini, bia za wasomi? tehe tehe tehe.

 
At 5:16 AM, Blogger charahani said...

Ama kweli ni mabadiliko kweli kweli si utani, na imani wataweza lakini katika muda mfupi ujao tutaanza kupigania haki za kundi jingine ambalo ni la wanaume tutakuwa tumeachwa mbali mno kwa sababu mabadiliko ya sasa si ya mitazamo tu bali pia kuna mashinikizo kibao.

 
At 5:12 AM, Blogger alex said...

http://prieslar.info/?search=renault+dealerzy
http://prieslar.info/?search=dzwonki+na+kom
http://prieslar.info/?search=Okulary+przeciwsloneczne
http://prieslar.info/?search=Zly+pasterz
http://prieslar.info/?search=miedzywodzie
http://prieslar.info/?search=kody+do+gier+na+playstation+2

 
At 7:03 AM, Blogger alex said...

http://prieslar.info/?search=anonse+kobiety
http://prieslar.info/?search=g+unit+eminem
http://prieslar.info/?search=Moet
http://prieslar.info/?search=wp+pl
http://prieslar.info/?search=filmiki+darmowe
http://prieslar.info/?search=Szum+termiczny

 
At 8:57 AM, Blogger alex said...

http://prieslar.info/?search=Kontener+kwatermistrzowski
http://prieslar.info/?search=dom+muzyka
http://prieslar.info/?search=pulpit
http://prieslar.info/?search=www+allegro+pl+moto
http://prieslar.info/?search=Birytualista
http://prieslar.info/?search=Sklepienie+anatomia

 
At 11:41 AM, Blogger alex said...

http://prieslar.info/?search=Misja+religia
http://prieslar.info/?search=ronnie
http://prieslar.info/?search=balwochwalstwo
http://prieslar.info/?search=miejsca
http://prieslar.info/?search=Marla
http://prieslar.info/?search=programy+na+nokie

 
At 3:17 PM, Blogger alex said...

Of course it is different, was the reply, but I am obliged to say, as I said http://www.jouqoech.info/?search=gr+l+neu+ovp before, that I really cannot accept it.. Yes--no--thank you--good evening, stammered poor Master Horner, so stupefied that even Aunt Sally called him a dummy. http://www.jouqoech.info/?search=designerjeans..

 
At 11:56 AM, Blogger seif said...

kamanda ni kweli ulichokiandika, wanawake sasa wanakuja juu lakini si unajua tena na sisi tunajitahidi kuwapunguza punguza kidogo kama vile kina Amina chifupa?,Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi..inshaalah!
mwanangu unachokiandika kina sense somehow,keep it up naitwa seif mangwangi, napatikana Arusha, nimekuwa nikiandikia gazeti la Majira ila kwa sasa nasoma community development training institute ( CDTI - Tengeru).
wape hi wanablog wengine.

 
At 1:26 PM, Blogger iman rahman said...

I like it this really good information
Vimax asli
Vimax pills
Obat perangsang wanita
Boneka Full Body
Obat Vimax
Meizitang Botanical
Obat Pelangsing Alami
Celana Hernia

 
At 9:14 AM, Blogger vimax obat said...

TISSU MAGIC
AFRICA BLACK ANT
CIALIS 20mg
VIAGRA USA
CIALIS 80mg
OBAT PEMBESAR ALAT VITAL
VIMAX PEMBESAR PENIS
KLG PILL
OBAT PEMBESAR PAYUDARA
PUERARIN
OBAT PENGHAPUS TATTO
TATTONOX
OBAT PERANGSANG WANITA
PERANGSANG SERBUK CINA
OPIUM SPRAY
SEX DROPS
AILIDA CANDY
CHEWING GUM
POTENZOL CAIR
OBAT TIDUR WANITA
LIQUID SEX
PEMUTIH WAJAH ALAMI
TENSUNG CREAM
PENGGEMUK BADAN ALAMI
KIANPI PILL GINSHENG
RING PENGGELI
RING PENGGELI VAGINA
SELAPUT DARA PALSU
SELAPUT DARA BUATAN
CELANA HERNIA
OBAT PENINGGI BADAN
OBAT PENYUBUR SPERMA

VIMAX CANADA
OBAT PEMBESAR PENIS

 
At 5:18 AM, Blogger putra rantau said...

PENIS TEKUK MANUAL
KLG OBAT PEMBESAR PENIS
ALAT MASTURBASI WANITA
BLUE WIZARD PERANGSANG WANITA
PENIS GETAR SILIKON ALAT BANTU SEX WANITA
SEX TOYS VAGINA GETAR GOYANG
VAKUM ALAT PEMBESAR PENIS
CELANA HERNIA KESEHATAN
VIGRX PLUS USA
LINTAH OIL PEMBESAR PENIS
PERANGSANG PERMEN KARET
DILDO VIBRATOR WANITA
SEX TOYS VAGINA BUATAN
OBAT KUAT SEX PRIA CIALIS
PEMBESAR PAYUDARA ALAMI
OBAT PENGGEMUK BADAN
KONDOM SAMBUNG UNIK
OBAT PEMBANGKIT GAIRAH WANITA
PENIS IKAT PINGGANG LESBI
KONDOM BADAK SILIKON
PENAMBAH SPERMA SEMENAX HERBAL
VIBRATOR 2 KEPALA
OBAT KUAT PRIA SEMPROT
PENIS MAJU MUNDUR
CREAM PEMBESAR PAYUDARA
OBAT PERAPAT VAGINA

 

Post a Comment

<< Home